Mch Dkt. Albrecht Philips kutoka Kanisa la Westphalia (Evangelical Church of Westphalia) Ujerumani pamoja na msafara aliombatana nao, wamehitimisha ziara yao ya siku mbili ya kuitembelea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), ikiwa ni pamoja na baadhi ya vituo vinavyo milikiwa na KKKT-DKMs, kwa lengo la kuona vituo hivyo vinavyofanya kazi ili kuweka nguvu ya pamoja katika kuviboresha ili viendane na wakati.



Na leo tarehe 08/07/2024 walitembelea Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, yaliyopo Lushoto Tanga, walipata nafasi ya kusalimiana na Wafanyakazi wa Ofisi Kuu na baada ya hapo walipata nafasi pia ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wao Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.

Msafara huo umetamatisha ziara ya siku mbili kwa kutembelea Makazi ya Askofu, Irente View pamoja na Hoteli ya Irente Farm.