Msaidizi wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju amesema kuwa kutokana na uwepo wa mmomonyoko wa maadili katika jamii Kanisa limeona ni vema kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wainjilisti wa Dayosisi ili wakawe chachu na kutatua changamoto hiyo katika jamii.
Msaidizi wa Askofu Mch.Michael Kanju ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Elimu ya Kikristo pamoja na Maadili yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Utondolo Lushoto Tanga yanayo jumuisha wainjilisti 15 kutoka katika Mjimbo matano ya Dayosisi, mafunzo hayo yatafanyika kwa majuma manne.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Bi.Ingrid Walz kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya KKKT Arusha amesema kuwa miongoni mwa mambo yatakayofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na kuwajengea uwezo Wainjilisti kuzijua mbinu mbalimbali za kufundishia pamoja na namna bora ya uendeshaji wa semina ambapo ameongeza kuwa mara baada ya mafunzo Wainjilisti hao watakuwa na uwezo wa kwenda kufundisha Jamii, Watoto wa Shule ya Jumapili pamoja na Shule za msingi na Sekondari.
Kwa upande wake mratibu Idira ya Elimu ya Kikristo pamoja na Uwakili Mch. Emmanuel Mweta ameweka wazi kuwa ni imani yake mara baada ya mafunzo hayo Wainjiliti hao watakuwa msaada mkubwa kwani kupia mafundisho sahihi watakayo yatoa kwa wanafunzi katika shule na maeneo mbalimbali yatasaidia kuijenga jamii yenye maadili mema.