Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, umeupongeza uongozi na wafanyakazi wa shamba la Irente Farm kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka kuongeza juhudi ili shamba hilo linalomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki lizalishe zaidi kulingana na ukubwa wake.

Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake ya siku nzima ya leo tarehe 25/07/2024 ya kutembelea shamba hilo kwa lengo la kujionea kwa macho kazi ambazo zinafanyika  na utekelezwaji wa majukumu na shuhuli za kila siku zinazofanyika katika Shamba hilo.

Mbali na pongezi hizo Baba Askofu Dkt. Mbilu, amesema kuwa ukubwa wa hekari 507 za shamba hilo ni wazi kuwa uzalisha wa bidhaa nyingi unahitajika ukiambatana na kutafuta soko la uhakika ila mazao yanayopatikana yaweze kwenda kwenye soko la uhakika na kwa wakati.

Alisema kuwa ni kweli kuna uwepo wa taarifa mbalimbali ambazo huwa zinawasilishwa kwa Viongozi kupitia vikao mbalimbali ila sasa ameona ni vema kutembelea shamba hilo na kujionea yeye mwenyewe kwa macho ni nini kinafanyika zoezi ambalo litakuwa endelevu katika maeneo mengine ya Dayosisi .

Huu ni mwendelezo wa ziara za Baba Askofu anazozifanya katika Vituo Sharika na maeneo mbalimbali ya Dayosisi kwa lengo la kujiridhisha na kujionea kazi mbalimbali zinavyofanyika katika maeneo hayo ili kuona sehemu ambazo zinahitaji nguvu ya Dayosisi ili kusaidia katika utekelezaji. Na leo akiwa katika Shamba la Irente Farm aliojionea mradi wa Ng’ombe na kupata taarifa la ongezeko la maziwa ambapo mbali ya ongezeko hilo ametoa ushauri wa kutafutwa kwa Ng’ombe wa kisasa zaidi.

“Soko la maziwa lipo kwa kiasi hiki cha lita za maziwa zinazo patikana hapa nashauri ni heri kuwa na Ng’ombe wachache wa maziwa wenye uwezo wa kutoa maziwa kwa wingi, mambo yote tunayofanya lazima tuyafanye kwa ukubwa wake na kwa jicho la kidayosisi.Alisema Askofu Dkt.Mbilu.

Mradi wa Nguruwe ni moja ya miradi iliyotembelewa na mradi huu unaendelea vizuri pamoja na mradi wa zao la parachichi, mradi wa nyuki ukiwa na jumla ya mizinga 24 pia unafanya zivuri, na hekari 16 za zao la kahawa zimetembelewa ambapo katika miradi hii uongozi wa Shamba la Irente Farm umetakiwa kufanya mambo katika ukubwa wake.

Irente Farm inajishughulisha na masuala ya utalii ikiwemo misitu midogo lodge ya kulaza wageni,restaurant kwaajili ya chakula, viwanda vidogovidogo vya usindikaji maziwa  ambavyo vinatoa bidhaa za cheese aina ya Gauda,cheda, mozzarella na butter pia husindika yoghurt na cream cheese au cottage cheese, kwenye matunda husindika jam za aina mbalimbali zikiwemo plum jam, loquat, Mulberry jam, mango chutney  passion jam, na passion juice, vilevile huoka mikate ya rye au brown bread na kutumika katika chakula cha asili cha Irente Farm kiitwacho farm lunch au picnic lunch.

Vilevile hujishughulisha na kilimo cha mbogamboga na ufugaji wa Ng'ombe wa maziwa na nguruwe, unga wa ngano aina ya rye pia unapatikana Irente farm.

KWA MAWASILIANO WASILIANA     Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. simu +255788 503 002  Tovuti: https://www.irentefarmlodge.com/