HABARI KWA UFUPI TANGA
HABARI KWA UFUPI
Ibada ya Jumapili siku ya Bwana ya 9 baada ya utatu aliyofanyika KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Jimbo la Pwani Usharika wa Pongwe Mtaa wa Diary tarehe 28/07/2024. Ibada ilikuwa na matendo makuu mbalimbali ikiwemo uwekwaji wa Jiwe la Msingi la Kanisa Pamoja na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Mtaa huo.
Ibada iliongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Dayosisi akiwemo Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu, CP Suzan Kaganda, Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe. Frederick Lowassa Pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi.
Siku ya leo keshi Tsh. 12,906,000 kimechangishwa ikiwa pesa taslimu ni Tsh. 3,554,400 huku kukiwa na ahadi ya mifuko ya cement 325, kamati ya Ujenzi wa Kanisa hilo imetoa kiasi cha Tsh. 100,000,000 na hivyo Jumla ya Tsh. 112, 906,000 kimepatikana.
Mtaa huu ulikua ni miongoni mwa jumuiya za Mtaa wa Kilapula, ilikua inaitwa Jumuiya ya Yeriko Diary, baada ya kuona changamoto ya umbali toka hapa kwenda Ibadani Mtaa wa Kilapula na changamoto kubwa tunayoipata hasa wakati wa mvua, ndipo wazo la kuanzisha Mtaa lilipokuja, hivyo wazee wa Kanisa wa jumuiya hii ya Diary Yeriko chini ya uongozi wa Mwinjilsti Yohana Zayumba walipo pata wazo wa kutafuta mahali pa kuabudia.
Mhasham askofu, Wazee hao pamoja na Mwinjilisti wakaona ipo sababu ya kutafuta eneo la kujenga Kanisa, ndipo jitihada mbalimbali zilifanyika kupata eneo lakini zilishindikana kutokana na upungufu wa fedha. Ndipo likapatikana wazo la kumuona Baba Yetu Dkt. Vicent Mhada kwa ajili ya kumuomba atoe eneo la kujenga Kanisa, na Baba yetu bila hiyana Baba alitupatia eneo la ekari moja kwa ajili ya Kanisa na nyumba ya mtumishi, pia Baba aliahidi kutoa ushiriano wa kutosha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la muda na Kanisa la kudumu.
Na tulianza Ibada eneo hili tar 08.09.2023 kama Mtaa sasa wa Yeriko Diary chini ya Mchungaji Jonathan Hiza. Na baadaye wanamtaa walipendekeza Mtaa libaki la asili tu, yaa Mtaa wa Diary. Mhasham Askofu, baba yetu Mzee daktari Vicent Mhada amekua akijitoa hata katika kanisa hilo la muda yeye amekua msaada mkubwa pia kwenye ujenzi wake mpaka hatua hiyo linavyoonekana, Mhasham Askofu Mtaa huu una jumla ya Wakristo 30.
Alisema Mwenyekiti wa Jengo la Kanisa Sia Naynge wakati anasoma Risala fupi ya Uwekwaji wa Jiwe la Msingi na Ujenzi wa Kanisa hilo. Aliongeza kuwa katikati ya mwezi wa January wazee wa Kanisa wakiwemo mzee Rhodes Nyange, Aminael Nikombolwe (Mama Lea), Neema Juma, na Rose Nduta pamoja na Mchungaj na mwinjisti walimtembelea Baba Daktari Vicent Mhada nyumbani kwake, na kwenye majadiliano mzee aliahidi kuungana na Wakristo wote wa Mtaa kujenga Kanisa kubwa na la kisasa kama linavyo onekana kwenye bango. Baba yetu Dactari Vicenti Mhada alipendekeza kuandaa harambee (fund rising). Ambapo leo ndiyo tarehe ambayo Mungu ametupa siku ya harambee hii.