HABARI KWA UFUPI:
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewakumbusha Wakristo kuishi maisha ya kumpendeza Mungu ili wawe na mwisho mwema. Askofu Dkt.Mbilu ametoa wito huo katika Ibada ya Mazishi ya Marehemu Mzee Dastan Mazimu yaliyofanyika katika Usharika wa Bumbuli tarehe 27/07/2024.
Marehemu Mzee Dastan Mazimu alizaliwa mnamo tarehe 05/12/1943 katifa Kijiji cha Kwag'wenda kilichopo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Wakati wa uhai wake marehemu Mzee Dastan Mazimu alishiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi, kijamii, na kiimani. na atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika elimu kwa kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Bangala akiwa fundi mkuu katiak ujenzi huo.
Pia Marehemu atakumbukwa sana kwani alikuwa mmoja wa watu waliofanikisha ujenzi wa Kanisa Kuu Lushoto .pamoja na ujenzi wa majengo mengine kama vile Hospitali ya Bumbuli inayomilikiwa na KKKT-DKMs. Marehemu Mzee Dasani Mazimu aliitwa mbinguni siku ya tarehe 23/07/2024 majira ya saa 8 maçhana katika Hostpitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila wakati akiwa anaendelea kupokea matibabu. Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, unaendelea kutoa pole kwa ndugu rafiki na jamaa wote walioguswa na msiba huu, Bwana ametoa Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.