KATIKA PICHA: Mkuu mpya wa Wilaya ya Lushoto Bw. Zephania Stephan Sumaye  leo tarehe 29/08/2024 ametembelea Ofisi za Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yaliyopo Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga kwa lengo la kujitambulisha kwa Uongozi wa Dayosisi. Bw. Zephania  Sumaye alipokelewa na watumishi wa Ofisi Kuu ya KKKT-DKMs na kupata nafasi ya kufanya mazungumzo na  mwenyeji wake Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.

 

MKUU MPYA WA WILAYA YA LUSHOTO BW. ZEPHANIA STEPHAN SUMAYE  AKISAINI KITABU CHA WAGENI- OFISI YA ASKOFU KKKT-DKMs

 

 

 

Mkuu  wa Wilaya ya Lushoto Bw. Zephania Stephan Sumaye, akisalimiana na Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs, Dean Michael Mlondakweli Kanju.