KATIKA PICHA IBADA YA KUWEKWA WAKFU NA KUINGIZWA KAZINI KWA ASKOFU BRYAN PENMAN LEO TAREHE 14/09/2024.Ibada hii ya kuingizwa kazini kwa Askofu Mch. Bryan J. Penman imefanyika katika Usharika wa Kanisa Kuu la Philadelphia (Philadelphia Episcopal Cathedral) na iliongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri MAREKANI - (ELCA), Bishop Elizabeth Eaton.
 
Askofu Penman anakuwa Askofu wa 6 wa Dayosisi rafiki ya Southeastern Pennsylvania Synod-MAREKANI. Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, kwa mualiko maalum kutoka Dayosisi rafiki ya Southeastern Pennsylvania ameshiriki Ibada hii ya kuingizwa kazini kwa Askofu Bryan J. Penman.
Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akiwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri MAREKANI - (ELCA), Bishop Elizabeth Eaton.
Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akiwa nje ya Kanisa la  FAITH IMMANUEL LUTHERAN CHURCH IN PENNSYLVANIA ambapo aliongoza Ibada ya Jumapili ya tarehe 15/09/2024.