KATIKA PICHA KUTOKA JIMBO LA KASKAZINI USHARIKA WA KIRETI MTAA WA MPANDA: Ibada ya Jumapili ya leo tarehe 06/10/2024 iliyoambatana na Kubarikiwa kwa Vijana wa Kipaimara 133 na watu wazima 3 kubatizwa iliongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.

Vijana waliobariki katika kuonesha utayari wa kuchangia Deni la Dayosisi walichangia kiasi cha shilingi 665,000 na kuwaomba wazazi na walezi kuwaunga mkono na baada ya kuungwa mkoni kiasi cha Tsh. 2,066,400 kilipatikana.

Katika kuendelea kudumisha urafiki kati ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Dayosisi rafiki ya Lund Sweden Usharika wa Kireti wametembelewa na marafiki zao kutoka Usharika wa Örkelljunga Dayosisi ya Lund Sweden na wameshiriki katika Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Usharika huo wa Kireti Mtaa wa Mpanda.


Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii
INSTAGRAM - / elctned
FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese
FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese
YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV
WEBSITE : https://elctned.org/
KWA MAONI NA USHAURI:
Simu : +255 743 399 798