Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu, ameongoza Ibada ya kuwabariki Vijana wa Kipaimara,uwekwaji wa jiwe la msingi la nyumba ya mtumishi pamoja na Ubatizo, Ibada iliyofanyika katika Jimbo la Kusini Usharika wa Bumbuli leo tarehe 13/10/2024.
Vijana wapatao 128 walibarikiwa na mmoja kati yao kubatizwa. Katika kuunga mkono jitihada za Askofu Dkt. Mbilu katika ulipaji wa deni la Dayosisi Vijana hao walichangia kiasi Tsh.1,300,000/=) na baadae waliungwa mkono na Washarika waliohudhuria katika Ibada hiyo na kuifanya jumla ya Tsh. 1,712,250/=.
Katika Ibada hiyo Askofu Dkt. Mbilu aliendesha harambee ndogo ya ujenzi wa Kanisa linaloendelea kujengwa Usharikani hapo ambapo kiasi cha Tsh 5,100,000/= kilipatika ambapo kati kuunga mkono ujenzi wa Kanisa unaoendelea Usharikani hapo Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mh. January Makamba ambaye alishiriki katika Ibada hiyo alichangia kiasi cha Tsh.2,000,000.
Askofu Dkt. Mbilu aliambatana na msaidizi wake Mch. Michael Mlondakweli Kanju, Katibu Mkuu wa Dayosisi Mwl. Julius Samwel Madiga,Mkurugenzi wa Huduma za Jamii Mwl. Afizai Vuliva na Mkurugenzi wa Uchumi na Mipango Bi. Pendo Lauo.