Ufunuo 14:13“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

KATIKA PICHA:Ibada ya mazishi ya Bibi. Elise David Ngome, iliyofanyika leo tarehe 28/01/2025 katika Jimbo la Kusini Usharika wa Mgwashi na kuongozwa na msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju akishirikiana na Mkuu wa Jimbo la Kusini Mch. Issai Mweta.

Marehemu Bibi Elise Ngome ambaye pia ni mke wa Marehemu Mchungaji David Ngoma aliitwa mbinguni tarehe 26/01/2025.Marehemu Bibi Elise Ngome ambaye alizaliwa mwaka 1938, mbali na kazi mbalimbali alizojihusisha nazo katika maisha yake aliweza kuwahudumia washarika wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki katika sharika mbalimbali ambazo walihudumu pamoja na mume wake Marehemu Mchungaji David Ngoma.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,chini ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, unaendelea kutoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na marafiki popotepale walipo.
BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na lihimidiwe.

