Print

Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii KUPITIA COMPASSION INATANGAZA NAFASI MOJA YA MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA (CHILD AND YOUTH DEVELOPMENT CENTER COORDINATOR (CYDC).

Utangulizi Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana ni mwajiriwa wa Kanisa na atatumika katika Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana (KKKT – MKATA – TZ1211) kilichopo Sindeni – Wilaya ya Handeni.

 1.1 MAJUKUMU

1.2 SIFA ZA MRATIBU WA KITUO CHA MAENDELEO YA MTOTO NA KIJANA ELIMU:

Shahada ya Kwanza (kutoka kwenye Chuo kinachotambulika/kukubalika na Serikali).

Elimu katika maeneo ya Uongozi/Utawala, Usimamizi wa biashara, Maendeleo ya jamii, Maendeleo ya watoto, Theolojia, Ualimu na Sosholojia

1.3 NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.

Maombi yote yatumwe kwa  

Katibu Mkuu KKKT-DKMs
S.L.P 10,
LUSHOTO TANGA
Kupitia email ya
:  This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Hits: 6061