Print

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amefungua rasmi kikao cha tathmini kwa kazi zilizotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2025.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika tarehe 12/02/2026 katika Hoteli ya Tumaini Mbuyukenda, Jijini Tanga, Askofu Dkt. Mbilu amesema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kuweka msingi imara kwa watumishi kutambua walipotoka, walipo na wanakoelekea katika utendaji wao wa kazi. Amesisitiza kuwa tathmini ni nyenzo muhimu katika kupima mafanikio, kubaini changamoto na kupanga mikakati madhubuti ya kuboresha utendaji kwa siku zijazo.

Aidha, Askofu Dkt.Mbilu ameeleza kuwa kikao hicho ni semina elekezi yenye dhima ya kujengeana uwezo wa kujitathmini, kujikosoa na kujirekebisha pale panapohitajika. Ameongeza kuwa kupitia semina hiyo, washiriki watapata fursa ya kukumbushana wajibu wao pamoja na kuongeza bidii katika utekelezaji wa majukumu ili kupunguza changamoto na kufikia malengo yaliyowekwa.

Katika hotuba yake ya ufunguza, Askofu Dkt. Mbilu ametoa pongezi kwa watumishi kwa utendaji mzuri wa kazi katika maeneo mbalimbali ndani ya Dayosisi, akisema mafanikio yaliyopatikana ni matokeo ya ushirikiano, uwajibikaji pamoja na kujituma.

Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo Kauli Mbiu ya Dayosisi ya “Kasi Tofauti”, akitaka ionekane wazi katika utendaji wa kila siku. Amefafanua kuwa kasi hiyo inapaswa kuambatana na Uwazi, kuzingatia Viwango vinavyotakiwa, pamoja na Umakini katika utekelezaji wa majukumu, ikiwemo utoaji wa taarifa sahihi katika ngazi zote ndani ya Dayosisi.

Kwa ujumla, kikao hicho cha tathmini kinatarajiwa kuwa chachu ya maboresho zaidi katika utendaji kazi, huku kikilenga kuimarisha uwajibikaji na kuongeza ufanisi kwa manufaa ya Dayosisi na jamii kwa ujumla.

Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii

INSTAGRAM - / elctned

FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese

FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese

YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV

WEBSITE: www.elctned.org

KWA MAONI NA USHAURI:

Simu : +255 743 399 798

 

Hits: 42