Print

Leo tarehe 01/04/2026, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amepokea ugeni kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Makao Makuu ya Ofisi za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka makao makuu ya NSSF Dar es Salaam, Ndugu Omary K. Mziya.

Katika mazungumzo yao, pande zote mbili zimejadili kwa kina namna Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, kama mdau muhimu wa maendeleo inavyoendelea kushirikiana vyema na NSSF. Ushirikiano huo umeelezwa kuwa na mchango mkubwa.

Ndugu Omary K. Mziya alieleza kufurahishwa kwake na mapokezi pamoja na mazungumzo yenye tija aliyoyapata kutoka kwa uongozi wa Dayosisi chini ya uongozi wa Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu. Alisisitiza kuwa NSSF itaendelea kushirikiana kwa karibu na Dayosisi ili kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanafikiwa.

Kwa upande wake, Askofu Dkt. Mbilu alishukuru ujio wa ugeni huo na kupongeza ushirikiano uliopo, akiahidi kuendelea kuimarisha mahusiano hayo.

Hits: 855