
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI
Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu yake Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT.
Dayosisi hii inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ni Taasisi ya dini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii inatangaza nafasi moja ya kazi ya MENEJA WA SHAMBA KATIKA KITUO CHAKE CHA IRENTE FARM.
Shamba la Irente Farm lenye ukubwa wa ekari (acres) 507 ni Kituo cha mfano cha kilimo endelevu kinacholenga kuendeleza uzalishaji wa kisasa, kuongeza tija, na kuchangia maendeleo katika Kanisa na jamii kupitia mbinu bora za kilimo na ufugaji. Ili kuimarisha ufanisi na ubora wa huduma zake ikiwemo huduma za Malazi (Hotel/Lodge), Kiwanda Kidogo cha Maziwa na Uzalishaji wa Jam na asali,Mazao ya misitu na nyuki,mikate ya asili ya Irente (Brown bread) ,pamoja na hayo, Irente Farm ni eneo ambalo linatunza uanuwai wa viumbe hai (biodiversity) kwa kuhifadhi miti ya asili hivyo basi Dayosisi inakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye sifa stahiki, uadilifu, na moyo wa kuhudumu katika nafasi hii.
Majukumu ya Kazi
- Kusimamia na kuratibu shughuli zote za kilimo na ufugaji katika Kituo cha Irente Farm.
- Kuandaa na kutekeleza mipango ya uzalishaji wa mazao na mifugo kwa ufanisi.
- Kusimamia matumizi sahihi ya rasilimali za shamba ikiwa ni pamoja na wafanyakazi, pembejeo na vifaa.
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu mbinu bora na za kisasa za kilimo na ufugaji.
- Kuandaa na kuwasilisha ripoti za maendeleo ya shughuli za shamba kwa uongozi husika.
- Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukuza na kuendeleza shughuli za kilimo endelevu.
- Kusimamia shughuli zote za hoteli iliyopo ndani ya shamba la Irente Farm
- Kusimamia ufuatiliaji wa taratibu za kisheria za Nchi,afya, Usalama, Mapato na Leseni
Sifa za Mwombaji
Mwombaji anatakiwa kuwa na:
- Shahada ya Kilimo (Agriculture) au Shahada ya Utawala wa Biashara au Taaluma nyinginezo zinazoendana na kazi hiyo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Uzoefu wa angalau miaka miwili (5) katika usimamizi wa shughuli za kilimo na/au ufugaji.
- Uwezo mzuri wa kutumia kompyuta na kuandaa ripoti za kitaalamu.
- Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea na kwa ushirikiano.
- Utayari wa kuishi na kufanya kazi Irente – Lushoto.
- Maadili mema ya Kikristo na moyo wa kuhudumu jamii.
Katibu Mkuu KKKT-DKMs
S.L.P 10,
LUSHOTO TANGA
Kupitia email : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
- Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, Wasifu wa mwombaji (Cv), Cheti cha kuzaliwa, na nakala za vyeti vyote vya ujuzi mbalimbali (kama unavyo).
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20/04/2026 saa 9:59 alasiri
- Waombaji watakaokidhi vigezo ndio watakaoitwa kwenye Usaili (Interview)
- Tarehe ya Usaili watajulishwa kwa njia ya simu/barua pepe.