MATUKIO KATIKA PICHA,IBADA YA NDOA KATI YA MHANDISI ANJAWE TURUCK NYAGAWA NA DKT. SARA MSAFIRI MBILU, IBADA IMEFANYIKA KATIKA USHARIKA WA MBEZI BEACH KKKT-DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI NA ILIONGOZWA NA MKUU WA KKKT MTEULE BABA ASKOFU DKT. ALEX MALASUSA . TAREHE 13,01,2024. DKT. SARA NI MTOTO WA KWANZA WA ASKOFU WA KKKT-DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI MCH DKT. MSAFIRI JOSEPH MBILU.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewataka Wazazi na Walezi wanapo upokea mwaka Mpya wa 2024 kuendelea kuwalea Watoto wao katika maadili mema kwani malezi bora ndiyo msingi wa kumsaidia Mtoto kutimiza malengo yake ya mbeleni.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewataka Wakristo kumpokea Yesu na kumkaribisha mioyoni mwao ili afanyike Nuru katika maisha yao na kuondoa giza na matendo yasiyofaa ambayo ni chukizo mbele za Mungu yaliyo tanda  katika ulimwengu na kuwasihi kumpokea  Yesu Kristo ambaye  ni  nuru ya ulimwengu.