Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  ametangaza uteuzi na mabadiliko madogo ya Wakuu wa Majimbo.Hii ni mara baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Utondolo Lushoto Tarehe 26-27/03/2024.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Mch Dkt Msafiri Joseph Mbilu, amewataka Vijana wa UKWATA Mkoa wa Tanga, kukubali kulelewa kiroho na kuwa mfano wa kuigwa wawapo shuleni kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo  kwa kufuata maadili mema na kuwa mstari wa mbele katika ufaulu mzuri darasani.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya KKKT-DKMs na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ameongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya KKKT-DKMs katika ukumbi wa mikutano, Utondolo Lushoto Tanga leo tarehe 26, Machi 2024.

Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi ifuatayo:

DAKTARI DARAJA LA II

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo vikuu/ Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Waombaji wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).