Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu anaendelea na ziara yake nchini Ujerumani, ambapo leo tarehe 06/03/2024 ametembelea Ofisi Kuu ya Kanisa la Kiinjili la Westphalia. Hili ni Kanisa lenye uhusiano Mkubwa na wa muda mrefu na Dayosisi yetu.
 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ambaye yupo ziarani nchini Ujerumani anaendelea na ziara yake na leo tarehe 05/03/2024 amekutana na kufanya mazungumzo na marafiki wa Dayosisi yetu. Katika picha  ni sehemu ya watumishi mbalimbali waliowahi kufanya kazi kwenye Hospitali ya Wagonjwa wa akili ya Lutindi Mental Hospital, inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, yupo ziarani nchini Ujerumani, ambapo akiwa nchini humo atashiriki Ibada ya kumuaga Katibu Mkuu wa chama Cha kiinjili Cha kimisioni (UEM) anayemaliza muda wake Mch.Volker Dally na kuingizwa kazini kwa Katibu Mkuu mpya wa UEM Mch. Dkt. Andar Parlindungan,ambaye awali  alikuwa Katibu mtendaji wa idaraya mafunzona uwezeshajiwa UEM.Ibada itafanyika tarehe 01/03/2024 

MATUKIO KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili siku ya Bwana ya 5 kabla ya Pasaka siku ya kuondoa ukatili, iliyofanyika KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto. Ibada hii ilikuwa na matendo mkuu mbalimbali ikiwemu tendo la kufunga mwaka wa Wanawake wa KKKT-DKMs uliozinduliwa 06/03/2022 pamoja na Jubilee ya miaka 25 ya utumishi ya Mchungaji Alice Kopwe na Mch Neema Kamendu.Ibada iliongozwa na inaongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu. 25/02/2024. Unaweza kutazama Ibada hii kwa kubonyeza link hii hapa chini.