
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo ameendelea kutambulishwa katika sharika mbalimbali za Dayosisi ambapo leo ameshiriki ibada ya Jumapili katika usharika wa Soni Jimbo la Kusini huku akiwataka waumini wa usharika huo kuanzisha miradi mbalimbali itakayowainua kiuchumi.

Askofu Mteule Mch. Dkt. Mbilu ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wateule akiwemo msaidizi wake Mch. Michael Kanju pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Mch. Godfrey Walalaze, amesema kuwa waumini wakiwa na miradi ambayo inawapatia kipato wataweza kushiriki vyema katika kuimarisha kazi za Dayosisi hususani katika nyanja za elimu, afya, na utumishi wa kiroho.
Sambamba na hayo Mch Dkt. Mbilu amesema kuwa Dayosisi imeamua kutoa punguzo kwa wanadayosisi watakaokwenda katika hospitali ya Bumbuli kwa ajili ya matibabu kuwa watapata punguzo la asilimia 10 ya gharama za matibabu.

Pamoja na hayo ameendelea kutoa mwaliko kwa wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika shule zinazomilikiwa na Dayosisi ikiwemo Lwandai na Bangala kwa kuwa watapata punguzo la asilimia 10 ya karo kama ilivyo kwa Hospitali ya Bumbuli.

“Napenda kutoa mwaliko kwa wanadayosisi kuwapeleka Watoto wao kusoma katika shule zetu za Bangala na Lwandai ambapo tumekubaliana kutakuwa na punguzo la asilimia 10 ya ada ilimradi tu uwe na namba ya ahadi”, Alisema Mch. Dkt. Mbilu.
Aidha Mch. Dkt. Mbilu amesema ataendelea kusimamia uimarishaji wa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu kwa kuwa kumekuwa na mafundisho potofu ambayo yanaleta mkanganyiko kwa waumini.
Pia Askofu Mteule amepata wasaa wa kuzindua kalenda ya Dayosisi inayoongozwa na Neno kuu la Dayosisi kutoka Zaburi 32:8 “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

Today the 17th of January, Bishop Elect Rev. Dr. Msafiri Mbilu led a worship service at Soni Parish (the head quarters of the Southern Superintendent) where he was introduced to the congregants.
In his speech, Bishop Elect Rev. Dr. Mbilu asserted that he, his Assistant, Acting General Secretary, members of the Executive Council of the Diocese and Superintendents of our respective Districts wholeheartedly accepted the responsibilities of serving God in this Diocese.
Explaining how they were committed to revamp various dormant works in the Diocese, Bishop Elect said that there were special discounts (10%) in our secondary schools and Bumbuli Hospital for all parishioners in the Diocese for respective services offered.
Talking about teachings of faith in the Diocese, Bishop Elect underscored His commitment to overseeing sound Lutheran Christian Doctrines since there is currently a wave of pervasive teachings in the Diocese and elsewhere.