Print

"Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza  yamekwisha kupita " UFUNUO 21:4.

 Kaimu Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mama Mzazi wa  Mch.Juliana Mahundo, Bi. Raheli Mahundo, kilichotokea  tarehe 05/11/2021.

 Ibada ya mzishi itafanyika siku ya Jumatatu tarehe 08/11/2021katika mtaa wa Mindu, Usharika wa Kwabada-Muheza.

 Uongozi unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.