
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt.Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 02/01/2022 ameongoza Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Mbaramo Mtaa wa Mlesa, Imekuwa siku ya Baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Mbaramo mtaa wa Mlesa. Ibada hiyo ilikuwa na matukio mbalimbali ikiwemo uwekwaji wa jiwe la msingi katika nyumba ya mtumishi pamoja na kufunguliwa kwa mnara wa kengele.


Kutokana na kalenda ya Matukio KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa mwaka 2022 matukio haya mawili yanaashiria kuzinduliwa rasmi kwa kalenda ya matukio mbalimbali yatakayo fanyika katika Dayosisi kwa mwaka huu.

Hata hivyo Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza wachungaji, Mch Dkt. Wiliam Kopwe na Mch. Alice Kopwe kwa kufikisha miaka 25 ya ndoa yao.Baba Askofu Dkt. Mbilu ndiye aliye ongoza sehemu ya Ibada hiyo ya shukrani ya jubilee hiyo katika Usharika wa Mbaramo Mtaa wa Mlesa.



