Print

 

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 19/01/2022 ameongoza Ibada ya mazishi ya Mchungaji mstaafu Anthony Danga Mndeme katika Usharika wa Mamba jimbo la Kusini.

Marehemu Mchungaji Anthoy Mndeme aliitwa mbinguni usiku wa tarehe 17/01/2022 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya  Lushoto.

Marehemu Mchungaji Mstaafu Anthoy Mndeme alianza masomo wa Uinjilisti mnamo mwaka 1968 hadi mwaka 1969 katika Chuo cha Biblia na Theologia mwika na mwaka 1971 hadi mwaka 1973 alisoma masoma ya uchungaji.Baada ya hapo alitumika katika sharika mbalimbali ndani ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Hata hivyo mara baada ya kustaafu aliendelea kuitumikia KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kutoa pole kwa,familia ya marehemu  Mchungaji Anthoy Mndeme ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.