Print

 

KKKT katika kutimiza wajibu wa kuwahudumia watu wake imekuwa ikitekeleza shughuli mbalimbali tangu kuanzishwa kwake kupitia mipango mbalimbali,mojawapo ya mipango hiyo ni mpango wa 2015 - 2026 ambao umefanyiwa tathmini na kupata mpango mpya wa 2022- 2026.

 Leo tarehe 01/02/2022 imefanyika warsha ya kushirikisha mpango huo mpya kwa viongozi na wafanyakazi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki katika ukumbi wa mikutano Utondolo-Lushoto kama sehemu ya kumilikisha mpango huo kwa Dayosisi zote za KKKT.

Mkurugenzi wa fedha na Utawala KKKT-DKMs CPA Peter Singano (wa kwanza kushoto),Naibu Katibu Mkuu Fedha na Utawala  KKKT CPA Loata Mungaya Laize(wa pili kutoka kushoto),Katibu Mkuu KKKT-DKMs Mch. Godfrey Tahona Walalaze,wa kwanza kutoka kulia pamoja na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu.
Naibu Katibu Mkuu Fedha na Utawala wa KKKT CPA Loata Mungaya Laizer ndiye aliyekuwa mwezeshaji katika warsha hiyo iliyo jumuisha wakuu wa majimbo,wakurugenzi, wakuu wa Idara na baadhi ya watumishi wa Ofisi kuu ya KKKT-DKMs ikiwa na lengo la kushirikishana mpango mkakati wa KKKT (2022-2026) na kupata mawazo mapya na shirikishi katika kuandaa mpango mkakati jumuishi wa Dayosisi utakaotekelezwa (2022-2026).


CPA Loata Laizer ametoa wito kwa Dayosisi zote za KKKT pamoja na vituo vya kazi za umoja kuhakikisha wanachukuwa mpango mkakati huo wa KKKT na kuoanisha na mpango mkakati walionao ili kuhakikisha Kanisa linakuwa na mpango mkakati mmoja ambao unatekelezeka ,ameongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na mpango mkakati mmoja ambao faida moja wapo ni kudumisha umoja wa kweli wa Kanisa.Umoja wa kweli utakwenda sambamba na mpango mmoja wenye mwelekeo mmoja utakao saidia kujenga Kanisa moja lenye nguvu ya pamoja,


Kwa upande mwingine Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amesema kuwa mpango mkakati huo wa KKKT utasaidia kuona umoja wa Kanisa kwa ujumla wake kwani kupanga pamoja,kufanyakazi kwa pamoja katika kipindi hiki cha miaka mitano kutasaidia kuona ni mambo gani yanaweza kufanyika kwa pamoja kama Kanisa,


Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Godfrey Walalaze kwa upande wake amesema kuwa kufanikiwa katika mpango mkakati huo ni lazima kupanga na kupanga ni hatua moja na kutimiza mpango ni hatua ya pili na kuutimiza sawasawa na makubaliano ni hatua iliyo bora naya muhimu zaidi hivyo anaamini kupitia hatua hiyo KKKT-DKMs itaungana kwa karibu na Dayosisi nyingine kuona Kanisa lina simama na kutimiza mipango yake ambayo imejiwekea kwa pamoja.