
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 05/02/2022 ameongoza semina elekezi kuelekea siku ya kuingizwa kazini kwa Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze,Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, CPA Peter John Singano pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki hapo kesho tarehe 06/02/2022.

