
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameendelea kuwa kumbusha Washarika wa Usharika wa Kange na Dayosisi kwa ujumla kuendela kuchangia Deni la Dayosisi na kusema kuwa taarifa ya michango hiyo itaendelea kutolewa kama ilivyo fanyika awali.

amewakumbusha Washarika hao leo tarehe 29/05/2022 ni siku ya Bwana kabla ya Pentekoste, SIKU YA CCT Neno Kuu (Sikia Kuomba kwetu) Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada ya Jumapili katika Jimbo la Pwani Usharika wa Kange na kuwasihi Washarika na Wanadayosisi kuona umuhimu wa kutoa sadaka ya CCT.

Ameongeza kuwa sadaka hiyo ni sehemu ya kujenga umoja katika CCT kwani pamoja na Wakristo kuwa na madhehebu yao tofauti bado CCT imeendelea kuwaleta pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali.

Aitha mchana wa leo linafanyika tamasha la siku ya CCT kwa ngazi ya Mkoa wa Tanga katika siku hii ya CCT katika Usharika wa Makorora na Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu ambaye pia ni Katibu wa CCT Mkoa wa Tanga amewakalibisha watu wote kufika na kushiriki katika tamasha hilo.

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) ambayo awali ilitambulika kwa jina la Tanganyika Missionary Council (TMC) ilianzishwa tarehe 23/01/1934 na hadi sasa imetimiza miaka 88. Jumuiya inamakanisa wanachama 12 na vyamba mbalimbali 14.

