Print

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

 Leo tarehe 30/05/2022 imefanyika Ibada ya mazishi ya Marehemu  Bibi,Hilgati A. Kika katika Usharika wa Makorora Jimbo la Pwani. Marehemu Bibi,Hilgati  Kika katika uhai wake alikuwa muimbaji wa kwaya Kuu KKKT-DKMs Usharika wa Makorora.

 

Marehemu Bibi,Hilgati ambaye pia ni mama mdogo wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, mwili wake umepumzishwa katika makaburi ya Bombo area Jijini Tanga.

Marehemu Bibi Hilgati alizaliwa tarehe 01/07/1948 katika Kijiji cha Kwang’wenda Wilayani Lushoto aliitwa mbinguni alfajiri ya tarehe 28/05/2022 katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga- Bombo.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kutoa pole kwa,familia ya marehemu,Kwaya Kuu Makorora,   ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.