
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameahidi kusimamia Maslahi na kuboresha hali ya kiutumishi kwa kila Mwinjilisti aliyeajiriwa na Dayosisi ikiwemo kuwekewa michango katika mfuko wa hifadhi ya jamii na kwamba hakuna Mwinjilisti atakae staafu bila ofisi ya Askofu kujua.

Askofu Dkt. Mbilu ameeleza hayo leo tarehe 09/06/2022 wakati akifungua semina ya siku nne iliyoandaliwa kwa Wainjilisti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yenye lengo la kuwajengea uwezo,inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benjamin Mkapa SEKOMU.

Mbali na hayo Askofu Dkt. Mbilu amewahimiza Wainjilisti hao kutumia muda wa kutosha katika kuandaa masomo na nyimbo kabla ya kutoa Mahubiri kwa watu wengine.
Pia amewataka kuachana na matumizi ya fimbo katika madarasa ya kipaimara na badala yake wabuni mbinu mbalimbali zitakazo saidia kufundisha neno la Mungu kwa ustadi.

Kwaupande wake Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Kanju amesema lengo na madhumuni ya semina hiyo ni kuwakusanya wainjilisti kwapamoja ili kuwaongezea uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika nyakati hizi zilizojaa mafundisho mengi ya uongo ya neno la Mungu

Kwaupande mwingine Mwinjilisti Eliya Yambazi Bila wa Jimbo la Kusini Usharika wa Manka na Neema Gogfrey Karata wa Usharika wa Irente mbali na kumshukuru Askofu kwa kuona umuhimu wa kuwakusanya pamoja na kuwajengea uwezo wameahidi kuyafanyia kazi mafundishoyote watakayoyapokea katika semina hiyo.
Semina hii ya Wainjilisti inafanyika ikiwa imepita zaidi ya miaka 20 tangu kuwapo semina kama hii na niyakwanza tangu Askofu Dkt. Mbilu kuingizwa kazini mwaka mmoja uliopita kuiongoza KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
