
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt. Fredrick Shoo leo tarehe 14/06/2022 amefungua semina elekezi kwa wasaidizi wa maaskofu inayofanyika makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Iringa.Maaskofu wapatao 27 wa Dayosisi za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wanahudhuria semina hiyo ya siku nne juu ya kazi za Mission na Uinjilishaji kwenye mazingira ya sasa yeye utandawazi na upotoshaji wa mafundisho sahihi ya neno la Mungu ndani ya Kanisa.
Akifungua semina hiyo Askofu Dkt. Shoo amesema Kanisa linapitia changamoto nyingi zikiwezo za tamaduni, mila, mfumo na mtazamo lakini ili kuyashinda hayo inabidi kusikia sauti ya Mungu inasema nini ndani ya Kanisa lake.
Mbali na hayo Mkuu wa Kanisa amesisitiza Dayosisi kusimamia mpango mkakati wa pamoja ambao utalileta Kanisa pamoja na kuimarisha umoja . Kwa upande wake Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Iringa Mch. Blastone Gaville mbali na kuwakaribisha wasaidizi wa maaskofu katika semina hiyo amesema kuwa anaamini semina hiyo itawaleta pamoja na kuwasaidia kubadilishana vipawa na karama alizowajalia Mungu.
Nae Msaidizi wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskanini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju amesema kuwa semina hiyo itawaunganisha Wachungaji wawe na muelekeo wa pamoja kuhusu mtazamo wa theolojia mbalimbali ambazo zinawapotosha watu katika nyakati hizi.