Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Fredrick O. Shoo ameelezea kufurahishwa kwake na waumini wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwajinsi walivyotambua umoja wa Kanisa ulivyo na nguvu katika kufanikisha kazi ya Mungu.
Mkuu huyo wa KKKT Askofu Dkt. Shoo ameeleza hayo leo tarehe 29/07/2022 akiwa katika Ibada ya Shukrani iliyofanyika kwenye Jimbo la Tambarare Usharika wa Korogwe ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashabiki.
Askofu Dkt. Shoo amesema inapendeza kuona jinsi mioyo ya wanadayosisi ya Kaskazini Mashabiki ilivyo imarika na kuheshimu umoja wa Kanisa kwa kujitoa kushiriki katika kazi mbalimbali.
Katika hatua nyingine Askofu Dkt. Shoo amewataka wanadayosisi ya Kaskazini Mashabiki kuendelee kuwaombea muda wote viongizi wa Dayosisi ili waendelee kuitenda vyema kazi ya Mungu bila kuchoka.
Pamoja na hayo Mkuu wa KKKT hakusita kumshukuru Askofu Dkt. Joseph Mbilu kwa kazi za diakonia ndani ya Dayosisi na kuongeza kuwa KKKT-DKMs imekuwa mfano katika Kanisa kwa kuwaendea wenye shida maalamu wanao hitaji msaada kwani huo ndio utambulisho wa Kanisa la KKKT.
Askofu Dkt. Shoo leo ametembelea Usharika wa Korogwe, Usharika wa Muheza na akiwasili katika Jimbo la Pwani ameanza ziara yake katika Usharika wa Pongwe na baadae aliwasili yalipo Makao Makuu ya Jimbo la Pwani Usharika wa Kana. Hapo kesho Askofu Dkt. Shoo anatazamiwa kuweka jiwe la Msingi la Kanisa Katika Usharika wa Makorora na kuongoza Ibada ya Kipaimara katika Usharika huo.