Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. Julius Madiga kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mzee Moses Gao Karata kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 10/06/2023 katika Hospitali ya Ocean Road-Dar Es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.
Marehemu Mzee Moses Karata ni Baba Mzazi wa Mchungaji William Karata wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Jimbo la Tambarare Usharika wa Mtonga.
Ibada ya Mazishi itafanyika jumanne ya tarehe 13/06/2023 katika Usharika wa Mtonga Korogwe saa tano.
Uongozi unatoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na lihimidiwe.