Print

PICHA ZA MATUKIO mbalimbali ya Ibada ya Mazishi ya Marehemu Mzee Moses Gao Karata, yaliyofanyika leo tarehe 13/06/2023 katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Mtonga, Ibada imeongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Kanju akishirikiana na Mkuu wa Jimbo la Tambarare, Mch Frank Mtangi.

Katika kipindi cha uhai wake (1980-1995) Marehemu Mzee Karata aliwahi kuwa mfanyakazi wa kiwanda cha uchapishaji Vuga Press (Vuga Press Publishing House) kinacho milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Marehemu Mzee Karata amefariki akiwa na  umri wa miaka 80  na mwili wake umepumzishwa katika makaburi yaliyopo katika eneo la Usharika wa Emao - Old Korogwe, Tanga.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kutoa pole kwa,familia ya marehemu Mzee Karata, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA libarikiwe.