
Askofu wa KKKT - Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru wana KKKT-DKMs pamoja na wadau wa maendeleo kwa namna walivyo jitoa na wanavyo endelea kujitoa katika uchangiaji wa deni linaloikabili Dayosisi.

Askofu Dkt. Mbilu ameongezakuwa taarifa ya makusanyo ya michango inayotolewa itakuwa inaendelea kutolewa kwa wakati na uwazi kama ilivyofanyika katika awamu ya kwanza na yapili ya uchangiaji wa deni hilo huku akisisitiza kuwa hakuna mali yoyote ya Dayosisi itakayouzwa endapo Wanadayosisi na marafiki wa ndani na nje wataingia kazini kwa uwaminifu kukabiliana na deni hilo.

Akitoa salamu zake kwenye Ibada ya Jumapili ya leo tarehe 25/06/2023 iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto ameongeza kuwa awamu hii ya tatu ya uchangiaji wa deni la Dayosisi ni awamu inayokuja na ombi maalum la utoaji wa mchango wa haraka ili kunusuru mali za Dayosisi zisipigwe mnada kwani wanaoidai Dayosisi ya Kaskazini Mashariki wameanza kukamata mali za Dayosisi ili kuzipiga mnada.

Ikumbukwe kuwa uongozi wa Askofu Dkt. Mbilu umerithi DENI la kiasi cha Tsh. 7,600,000,000 kutoka uongozi uliopita. Deni hili kubwa linatokana na mkopo uliochukuliwa CRDB, madeni ya malimbikizo ya mishahara na stahiki za watumishi wa kilichokuwa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University (SEKOMU), malimbikizo ya malipo ya Mifuko ya Kijamii.

Hadi sasa kwa kupitia michango mbalimbali ya Wanadayosisi na marafiki wa ndani na nje deni la CRDB kiasi cha takribani TZS. 1,200,000,000 (Bilion Moja na Milion Mia Mbili) limeshaa lipwa. na kwa sasa wale wengine wanaoidai Dayosisi wameshinda kesi na wamepewa kibali na mamlaka zinazo husika kukamata mali za Dayosisi na kuzipiga mnada.
Unaomba wewe utoe mchango wako ndani ya siku hizi chache ili kupunguza deni hili. Tunatanguliza shukrani zetu kwako. Pia tusaidie kuwashirikisha marafiki zako ili waungane nasi kukabiliana na deni hili.Namba za uchangiaji kwa njia ya mitandao ya simu ya Airtel na Tigo ni LIPA NAMBA 7122325 Jina la mpokeaji ni ELCT-NORTH EASTERN DIOCESE . Kwa njia ya Bank ya CRDB-
Jina la Akaunti ni ELCT-NORTH EASTERN DIOCESE

