
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ambaye yupo ziarani nchini Ujerumani anaendelea na ziara yake na leo tarehe 05/03/2024 amekutana na kufanya mazungumzo na marafiki wa Dayosisi yetu. Katika picha ni sehemu ya watumishi mbalimbali waliowahi kufanya kazi kwenye Hospitali ya Wagonjwa wa akili ya Lutindi Mental Hospital, inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.