Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, pamoja na msaidizi wake Mch. Michael Kanju, wameshiriki kwenye uchaguzi wa kumpata Askofu Mpya wa Sinodi rafiki ya Southeastern Pennsylvania, iliyoko Philadelphia nchini Marekani , ambapo uchaguzi huo uliofanyika leo tarehe 05/05/2024 umekamilika na Mch. Bryan Penman amechaguliwa kuwa Askofu Mteule akichukuwa nafasi ya mtangulizi wake
Askofu Dkt. Patricia Davenport aliyemaliza muda wake.

Katika uchaguzi huo Askofu Mteule Mch. Penman amepata ushindi dhidi ya mshindani wake wa karibu Mch. Karl Richard.

Mkutano wa uchaguzi ulisimamiwa na Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Marekani Deacon Sue E. Rothmeyer ambaye mara baada ya uchaguzi huo alimtakia baraka za Mungu Askofu Mteule Mch. Bryan katika wajibu alioitiwa wa kuiongoza Sinodi hiyo iliyo kiungo muhimu cha Kanisa hili lenye jumla ya Sinodi 65.

Katika sehemu ya salaam zake za kupokea wajibu huo Askofu Mteule Mch. Bryan ameahidi kuendeleza mahusiano mema katika Kanisa huku akikaza zaidi juu ya ushirikiano na Umoja wa Kanisa ndani na nje ya nchi.




