Uncategorised
- Details
HABARI KWA UFUPI
Wakristo wamekumbushwa kuendelea kumtumaini na kumtegema Mungu pale wanapo pata mafanikio katika maisha yao kwani katika dunia ya sasa wapo waliofanikiwa na mara baada ya kupata mafanikio hayo wakamsahau Mungu na kufuata njia zao, na kuamini kuwa mafanikio hayo wameyapata kwa nguvu zao.
Hayo yamesemwa na Jackson Msafiri Mbilu wakati akihubiri kwenye Ibada ya Jumapili ya leo tarehe 09/02/2025 iliyoongozwa na Vijana katika Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.” Ndugu zangu inasikitisha lakini ni uhalisia kuwa sisi binadamu sikuhizi tukifanikiwa katika maisha yetu, hatutaki kuwakumbuka kabisa wale waliotufikisha katika mafanikia. Tunawageuzia kisogo na kujifanya hatuwajui.”Alisema.
Ameongeza kuwa neno la Mungu ndiyo silaha na ngao katika maisha lakini inasikitisha katika ulimwengu wa sasa kuona watu wamekuwa wavivu wa kusoma neno la Mungu na kuna watu wanaoishi bili kumwamini mungu ameongeza kuwa wapo Wakristo, wanaofika kanisani ilimradi tu waoneka kuwa wamefika kanisani ili wakiulizwa na wengine waseme wameenda kanisani, hali inayopelekea kushindwa kujibu hata maswali marahisi yanayohusu Biblia.
Hata hivyo Jackson amewahimiza Wakristo kushiriki Ibada katika ukamilifu wake ili kuzivuna baraka za Mungu amesema litrugia sio Ibada kamili, muda wa mahubiri sio Ibada kamili au nzima, muda wa sadaka sio Ibada nzima, matangazo sio Ibada nzima bali Ibada kamili ni ile ambayo umeshiriki kuanzia mwanzo hadi baada ya mnada na hapo ndio unaweza ukasema umeshiriki Ibada katika ukamilifu wake.Yesu ndio tumaini letu sisi wanadamu tunapaswa kumfuata yeye, na kwakupitia maandiko matakatifu ya Mungu tunasikia neno lake na mafundisho yake sauti ya huyu Yesu tutaisikia kila siku kama tutapenda kukaa nyumbani mwa Bwana kulisoma Neno la Mungu kila siku na kila saa.
Katika Dayosisi yetu, KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Ibada zimeongozwa na vijana na katika Usharika wa Kanisa Kuu Ibada iliongozwa na Edison Kisaka pamoja na Jackson Mbilu.
Jackson Mbilu ambaye ndiye aliyehubiri ni Mtoto wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Dkt.Msafiri Joseph Mbilu ,ameeleze jinsi alivyokuwa anajiandaa na Ibada ya leo.“Moja wapo ya maandalizi Nilipokuwa ninaandaa haya mahubiri, Sasa pale nyumbani kwetu chatllon kuna ka ofisi cha baba ambayo anatumiaga kuandaa mahubiri sasa na mimi nikiwa ninayaandaa ya kwangu nikasema naenda kukaa pale pale. kwenye kiti kile kile angalau na mimi nipate upako na kujuwa nini cha kusema”. Alisema Jackson.
- Details





- Details
Shule za Sekondari za Lwandai na Bangala Junior Seminary, zinazomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), zimeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika November, 2024
Katika matokeo hayo, shule ya Lwandai imevutia zaidi baada ya kutoa mwanafunzi aliyepata alama za juu akiwa na daraja la kwanza lenye pointi saba (One ya 7), kitu kinachoashiria uwekezaji mkubwa katika elimu bora na juhudi za walimu pamoja na wanafunzi.
Kufuatia matokeo hayo Askofu wa KKKT-DKMs, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ,ametoa pongezi kwa walimu na wafanyakazi wa Shule hizo kwa kazi nzuri walioifanya huku akiahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili kuweka msingi imara wa mafanikio zaidi ya siku zijazo.
Kakita hatua nyingine Askofu Dkt. Mbilu, ametoa shukrani zake za dhati kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi kwa kukubali ombi la kila Usharika wa KKKT-DKMS kusomesha mwanafunzi mmoja katika Shule hizi.
“ninapoyatazama matokeo haya ya kishindo ya Shule zetu Lwandai na Bangala ninajikuta mdomo wazi nikimshangaa Mungu kwa jambo hili kubwa alilotutendea. Ninawapongeza ninyi wote kwa maamuzi yale magumu tuliyofanya kwenye kikao chetu cha kwanza cha tarehe 17.12.2020 kuwa kila Usharika usomeshe mwanafunzi mmoja kuanzia Januari 2021 ili kuondoa aibu ya Shule hizi kuwa na wanafunzi wachache wa kidato cha kwanza Lwandai 8 na Bangala 3. Hili limezaa matunda haya na kwa hakika Shule zetu zimefufuka. Hongereni sana.
Siku chache kabla ya Mtihani wa kidato cha Nne nilitembelea Shule zetu hizi kufanya maombi na watoto wetu na kuwapa kila mmoja kalamu ya kufanyia Mtihani kwa niaba yenu. Hakika Mungu amesikia maombi yetu na ametenda na ameamua KUTUPA RAHA. Nawapongeza ninyi Wajumbe wa Halmashauri Kuu, Wana KKKT-DKMS na wadau wote wa maendeleo kwa Ufadhili wao.
Nawapongeza Wazazi wa watoto hawa, Nawapongeza Wakuu wa Shule zetu, Walimu wote na watenda kazi wote kwa ufaulu huu wa hali ya juu sana. Tunazo hadi Divisheni One ya point 7. Nawapongeza watoto wetu kwa kufanya vizuri kwenye Mtihani Huu”Amesema Askofu Dkt. Mbilu.
Pamoja na hayo Askofu Dkt. Mbilu, amempogeza kipekee mwanafunzi Helena Frank Kaduma wa shule ya sekondari Lwandai kwa kupata ufaulu wa Division One ya point 7 ambapo mwanafunzi huyo amesomeshwa na Usharika wa Hale pamoja na mwanafunzi kutoka shule ya seminari ndogo ya Kilutheri Bangala,Dickson David Kika ambaye amepata ufaulu wa Division one ya 9 ambaye amesomeshwa na usharika wa Soni.
Matokeo haya mazuri yanaendeleza sifa nzuri ya shule hizi kama vituo vya elimu vinavyozalisha viongozi wa kesho walio na maarifa na maadili mema, na ujuzi unaohitajika kwa maendeleo ya Taifa. Sharika za KKKT-DKMS zitaendelea kuwasomesha vijana hawa kidato cha Tano na cha Sita. Mungu aendelee kutubariki tunapoyafanya makubwa haya. "BWANA AKASEMA, USO WANGU UTAKWENDA PAMOJA NAWE, NAMI NITAKUPA RAHA"(Kutoka 33:14).
- Details
HABARI KWA UFUPI: Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,amesema kuwa mipango ya uanzishwaji wa kozi ya muziki katika Taasisi ya Elimu ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) inaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na vifaa vitakavyo tumika katika kufundishia kuanza kupatikana.
Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 22/01/2025 akiwa katika Ofisi za Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yaliyopo Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga, mara baada ya kupokea ugeni wa marafiki kutoka Bethel Ujerumani.
Ugeni huu unaongozwa na Bw.Werner Jakob Blauth, ambaye alishaawahi kufanya kazi katika kituo cha Lutindi Mental Hospital kinachomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
Aidha Askofu Dkt. Mbilu, ameongeza kuwa ugeni huo umetembelea KKKT-Dayosisi Kaskazini Mashariki kwa lengo la kuona baadhi ya vituo vya Diakonia vya Dayosisi ikiwemo kituo cha Irente children's Home, Irente Rainbow School, Irente School for the Blind pamoja na Hospital ya wagonjwa wa akili (Lutindi Mental Hospital) ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika vituo hivyo.
Vifaa vilivyo pokelewa leo ni pamoja na Tarumbeta filimbi vikiwa ni alama tu ya vifaa vingine vingi vya muziki ambavyo vipo nchini Ujerumani vikiwa katika hatua za mwisho kusafirishwa kuja katika Dayosisi yetu.
Hata hivyo Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, amewashukuru wageni hao kwa mchango wao mkubwa wa kutoa vifaa hivyo vya muziki ikiwa ni ishara ya kuendelea kuonyesha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Dayosisi na marafiki hao kutoka Ujerumani.
Page 1 of 112