Tarehe 02/11/2024 Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, alipatanafasi ya kuitembelea SACCOS ya Tumaini KKKT Handeni Savings and credit co-operative Society Ltd, iliyopo katika Jimbo la Magharibi Usharika wa Handeni kwa lengo na kuona namna SACCOS hiyo inavyoendeshwa.
Pamoja na mambo mengine Baba Askofu mara baada ya kupokea taarifa ya SACCOS hiyo na yeye alijiunga huku akisema kuwa ni wakati sahihi kwa Washarika, Watu binafsi na Vikundi mbalimbali kujiuga na SACCOS hiyo ambayo inafanya vizuri.
Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) ni asasi za kifedha zinazoanzishwa, kumilikiwa na kuongozwa na wanachama kwa misingi ya kidemokrasia ili kuwasaidia kujifunza kuweka akiba na kuweza kupata mikopo kwa riba nafuu kutokana na akiba zao.
Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0623377559.