HABARI KWA UFUPI
Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Malasusa amewataka Wakurugenzi wa Taasisi za Kanisa kuwa wabunifu katika kuendesha Taasisi hizo pamoja na kujifunza kwa wengine ili kuongeza ufanisi na kuweza kufanya vizuri katika kutoa huduma bora kwenye jamii.
Askofu Dkt. Malasasusa ameyasema hayo tarehe 18/11/2024 akiwa jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya Wakuu wa Taasisi za Kanisa zikiwemo Hospitali, Shule, Hotel, Bank, vyombo vya Habari pamoja na Vyuo vinavyomilikiwa na KKKT.
Kwa pande wake Katibu Mkuu wa KKKT Bw. Rogath Lewis Mollel amesema warsha hiyo itakuwa endelevu ili kuhakikisha Taasisi za Kanisa zinakuwa Bora na zinaendeshwa kwa ufanisi na kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.
Washiriki wa warsha hiyo ambao ni wasimamizi wakuu wa taasisi za Kanisa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Upendo Media Bi. Neng'ida Johannes wamekiri kuwa warsha hiyo itawasaidia kuendelea kufanya kazi zao kwa ubora wa hali ya juu na kuzisaidia taasisi zao kupiga hatua zaidi.Hii ni mara ya pili kufanyika kwa Warsha hii ikiwa na lengo la kufanya Tathmini ya malengo waliyojiwekea na kuwajengea uwezo zaidi viongozi wa taasisi hizo ili kuboresha Utendaji na kutoa huduma bora zaidi kwa jamii.