Print

Kaimu katibu Mkuu Mch. Godfrey T. Walalaze leo tarehe 05/02/2021 amehitimisha Semina elekezi ya mafunzo ya kuimarisha Vituo vya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki iliyo anza jana Katika ukumbi wa mikutano Cathedral ambapo amegusia mambo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuzijua Kanuni, Sheria na Taratibu za Kazi.

Pamoja na hayo Mch Godfrey Walalaze amesema kuwa Vituo vya Dayosisi vinatakiwa kujiendesha hivyo ametoa miezi mitatu kwa kila kituo kuhakikisha kinajiendesha. Pia ameahidi kuwa Ofisi ya Katibu Mkuu pamoja na uongozi wa Dayosisi upo tayari kutoa ushirikiano kuhakikisha jambo hili linafanikiwa ,amewakumbusha wakuu wa vituo juu ya umuhimu wa kufahamu Taswira na Dhamira ya Dayosisi.

TASWIRA Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania- Dayosisi ya Kaskazini  Mashariki, ni Kanisa lililojengwa juu ya msingi imara, yaani Yesu Kristo.  Kwa njia ya Neno la Mungu lililoandikwa katika Agano la Kale na Agano Jipya na kwa Sakramenti Takatifu pamoja na maungamo ya Kilutheri, hukiri kuwa ni msingi wa pekee na usiokosea kwa mafundisho na maisha ya Kanisa.

DHAMIRA Kwa kufuata kielelezo cha Bwana Yesu katika Luka 4:18-19, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki inashuhudia Injili ya Mungu kama ilivyofunuliwa katika Yesu Kristo na kumhudumia mwanadamu kiroho, kiakili, kimwili na kijamii ili apate maendeleo yanayomwezesha kujitegemea.