Print
Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mzee Paul Kaijuka kilichotokea nyumbani kwake Korogwe tarehe 23/05/2022.
 
Marehemu Mzee Paul Kaijuka katika uhai wake aliwahi kuitumikia KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Masharika kama Mhasibu Mkuu na Mkaguzi wa ndani wa mahesabu ya Dayosisi kwa vipindi tofauti.
 
Mazishi yatafanyika siku ya Ijumaa tarehe 27/05/2022 yakitanguliwa na Misa fupi nyumbani kwake na baadae saa sita mchana itafanyika Misa ya Mazishi katika PAROKIA YA MTAKATIFU. AUGUSTINO MANUNDU-KOROGWE.
 
Uongozi unatoa pole kwa familia ya Marehemu Mzee Paul Kaijuka, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na lihimidiwe.