
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa Wainjilisti ni jeshi kubwa katika Dayosisi, linalofanya kazi kubwa na nzuri inayoonekana kwa kuwafikia wana Dayosisi kwa ukaribu zaidi.

Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 12/06/2022 kwenye Ibada ya Jumapili na kilele cha juma la Uinjilisti katika Dayosisi ambapo Wainjilisiti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki wapatao 211 wameshiriki kwenye Ibada hiyo iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto.

Hata hivyo Askofu Dkt. Mbilu hakusita kuwajulisha Wainjilisti na Wanadayosisi kwa ujumla juu ya ujio wa Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) ambacho kipombioni kukamilisha usajili wake ili kuanza udahili katika mwaka huu wa masomo wa 2022/2023.


Ikumbukwe kuwa Askofu Dkt. Mbilu alipata wasaa wa takribani siku nne ya kukaa na Wainjilisti wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwenye semina iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo Wainjilisti hao hasa katika nyakati hizi zilizo jaa mafundisho potofu ya neno la Mungu semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benjamin Mkapa SEKOMU ambapo pia Baba Askofu Dkt Msafiri Mbilu alipata nafasi ya kuwasikiliza Wainjilisti hao juu ya changamoto wanazo zipata na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi.


