Print

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amemtambulisha Katibu Mkuu Mpya wa KKKT-DKMs Mwl. Julius Samweli Madiga kwa Washarika wa Jimbo la Pwani hususani wa Usharika wa Kange.

Utambulisho huo ameufanya leo jumamosi ya tarehe 10/12/2022 kwenye Ibada ya ndoa kati ya Lucas Emmanuel Mtoi na Elizabeth Evod Kawishe iliyofanyika katika Usharika wa Kange. (Lucas Emmanuel Mtoi) - Ni mtoto wa Mch Emmanuel Mtoi mchungaji kiongozi wa Usharika wa Kange.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. JuliusĀ  Madiga ameendelea kuwaomba wanadayosisi waliopo ndani na nje ya Dayosisi kumuombea kwa Mungu ili atimize vema wajibu alioitiwa.

Ikumbukwekuwa Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, iliyoketi tarehe 04/11/2022 kwa kauli moja ilipitisha jina la Mwl. Julius Samweli Madiga kuwa ndiye Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Masharki kuanzia tarehe 15/11/2022.