
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ametoa wito kwa wachungaji na watumishi wengine wa Kanisa kuwatambua watu wenye shida ya kusikia (viziwi) ili wasiachwe na ujumbe wa neno la Mungu unapohubiriwa.

"Tutaendelea kuwapeleka wanafunzi wengine ikiwa ni wachungaji na watu wa taaluma mbalimbali kujifunza Lugha ya alama na ukalimani kwakuwa watu hawa wenye shida ya kusikia (VIZIWI) tunao katika makanisa yetu ili ujumbe wa neno la Mungu unapohubiriwa uweze kuwafikia.

Mch. Yohana Kakoa akipokea cheti kutoka kwa Baba Askofu Dkt. Mbilu.
Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 11/12/2022 kwenye Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Usharika wa Kana Tanga marabaada ya Mchungaji Yohana Kakoa aliyetumwa na KKKT-DKMs kuhudhuria mafunzo ya Lugha ya alama na ukalimani kuhitimu mafunzo yake katika mradi uliopo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ujulikanao kwa jina la Mradi wa KKKT Umisioni kwa Viziwi .
Naye Mchungaji wa KKKT-DKMs Yohana Kakoa mhitimu wa mafunzo hayo ameushukuru uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kumuamini na kumtuma kushiriki mafunzo hayo na ameahidi kuwatumikia viziwi na kuwapa ujumbe wa neno la Mungu kupitia elemu aliyoipata.

Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch. Thadeus Ketto
Kwa upande wake mwalimu wa Lugha ya alama na ukalimani kutoka mradi wa KKKT Umisioni kwa Viziwi ndugu Lazaro Kamba amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwaandaa watumishi wa Kanisa kuwahudumia viziwi na kujenga jamii jumuishi.

Askofu Dkt. Mbilu awali katika Ibada hiyo alimtambulisha Katibu Mkuu mpya wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mwl. Julius Samweli Madiga kwa washarika wa Usharika wa Kana nakuendelea kuwaomba kumpa ushirikiano ili aendelee kutimiza wajibu alioitiwa.


