
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amekuwa na ziara ya kikazi Nchini Hungary ambapo alihudhuria kikao cha kamati ya Ibada na Muziki ya Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF).

Wajibu wa Kamati hii ni kuratibu utaratibu mzima wa Ibada katika Mkutano Mkuu wa LWF utakaofanyika Krakow Poland mwezi Septemba mwaka huu. Baba Askofu Dkt. Mbilu ameshiriki kikao hicho cha wiki moja kilichofanyika kwenye mji wa Fót nje kidogo ya Budapest (Mji Mkuu wa Hungary).

Kamati hii iliundwa mnamo mwaka 2021 na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani ambayo makao makuu yake yapo Geneva Uswis. Kamati hii ina wajumbe kumi kutoka Ujerumani, Canada, Norway, Hungary, Poland, Hong Kong, USA, Brazil, Switzeland na Africa ambapo mjumbe muwakilishi ni Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu.

Baba Askofu Dkt. Mbilu, akiwa na Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Hungary, Askofu TAMAS FABINY