Print
 
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewataka Wakristo kuendelea kuwa kielelezo kwa wale wasiojua kweli ya Kristo kwa kumtumikia mungu kwa roho na kweli.
Askofu Dkt. Mbilu ametoa wito huo leo tarehe 23/04/2023 wakati akihubiri katika Ibada ya Jumapili ya pili iliyofanyika Katika Usharika Mteule wa Nywelo Jimbo la Kaskazini ambapo amesema ni jukumu la Wakrito kuifanya kazi ya Mungu kwa pamoja na kushirikiana na watumishi ilikuendelea kueneneza kweli ya neno la Mungu na kuepukana na mafundisho potofu ya neno la Mungu.
 
Askofu Dkt. Mbilu amesema ni lazima wakristo kutambua na kujihathariri na mafundisho ya uongo ambayo yanawasumbua waumini kwa kupewa visaidizi kama mafuta , vitambaa vyenye picha za manabii na mitume nakadhalika na badala yake wamwamini Yesu Kristo aliyekufa msalabani na kufufuka kwa ukombozi wa ulimwengu mzima.
 Aidha Askofu Dkt. Mbilu amewasii wakristo kuendelea kutunza uumbaji wa Mungu ikiwemo kutunza mazingira na kuepuka ukataji wa miti holela.
Awali Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu aliongoza Ibada ya Watoto wa Shule ya Jumapili katika Usharika huo Mteule wa Nywelo.