
KATIKA PICHA ni Ujumbe kutoka Tanzania uliohudhuria Mkutano wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani. Katikati ni Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa LWF Mch. Dkt.. Anne Burghadt akifuatiwa na Rais wa LWF Archibishop Musa Panti Filibus.

Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo akiwa na Rais wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani, Archbishop Musa Panti Filibus (Katikati) Pamoja na Askofu wa KKKT-DKMS Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.

Mkutano huu unaoendelea nchini Kenya ni Mkutano Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani kanda ya Afrika. Kwa kuwa mwaka huu utafanyika Mkutano Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani kwenye Mji wa Krakow nchini Poland, hivyo kila Bara wanapaswa kufanya Mkutano Mkuu. Hivyo Mkutano huu Mkuu umewakutanisha Walutheri wa Bara zima la Afrika na msafara kutoka KKKT unaongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt. Fredrick Shoo.
