Print

Kwa nyakati tofauti Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameahidi kuendelea kuhamasisha upandaji wa miti, utunzaji wa mazingira katika Dayosisi pamoja na maeneo mbalimbali sambamba na kutunza misitu ikiwemo  inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Jitihada hizi za Baba Askofu miongoni mwa faida zake ni pamoja na kulinda vyanzo vya maji, kuvuta mvua, kuwa makazi ya viumbe hai mbalimbali, kutoa nishati ya kuni, mkaa na kutoa mbao, miti pia husaidia kunyonya na kuhifadhi hewa ukaa inayozalishwa na binadamu kutokana na shughuli zake mbalimbali.

Sambamba na hayo Baba Askofu Dkt. Mbilu ameshiriki Mkutano wa Umoja wa vyama vya Kimissioni (Lutheran Mission Cooperation) uliofanyika katika hoteli ya Seashells Millennium Jijini Dar es Salaam mkutano ulifunguliwa tarehe 03/10/2023 na kufungwa leo tarehe 05/10/2023.

Mkutano huu umehudhuriwa na Maaskofu wa KKKT pamoja na Wawakilishi marafiki kutoka Ulaya na Marekani ukiwa na Ujumbe wenye tija ya Mabadiliko ya tabia ya Nchi kwani limekuwa  janga linaloikabili Dunia kwa sasa kutokana na uharibifu wa mazingira.

Neno kuu katika Mkutano huu ni kutoka kitabu cha Mwanzo 1:26-31.

“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi............................