Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza nakuwatakia baraka za Mungu katika masomo yao wanafunzi wanaoenda masomoni kwa mhula mpya wa masomo na wale ambao wanaendelea na masomo katika Chuo cha Biblia na Theolojia Mwika pamoja na Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira.
Baba Askofu amewakumbusha kuwa wanaenda kuiwakilisha KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na wanatumwa na Dayosisi kwa ujumla hivyo wakajitahidi kusoma kwa bidii na kujiepusha na mambo yasiyofaa, kusimamia yale ambayo niya Kanisa ili mwisho wa siku wafaulu vizuri na kuja kuitumikia Dayosisi.
Kwa kozi ya Theologia katika Chuo cha Biblia na Theolojia Mwika wanafunzi wanaoenda kusoma wapo wanne Josephat Samweli Mbilu,Tobias John Pazia,EsterVicent Mdoe pamoja na Peter Joseph Kakunya.
Wanafunzi wawili ambao ni Christina Robert Kaoneka pamoja na Ibahati Abraham Kassinge wao wanaenda kusoma kozi ya Shahada yaani Bachelor of Divinity katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kwa mwaka wa masomo 2023/2024.
