Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema uongozi wa Dayosisi unatambua mchango mkubwa wa walimu pamoja na watumishi waliopewa dhamana ya kutumika katika Taasisi za Elimu ndani ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

KATIKA PICHA:Mazishi ya Mama Askofu Elfriede Sebastian Kolowa iliyofanyika KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto leo tarehe 06/03/2025. Ibada hii iliongozwa na Mkuu wa KKKT Baba Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa.Marehemu, Bibi Elfriede Sebastian Kolowa alizaliwa tarehe 30 mwezi Juni mwaka 1934 huko Bumbuli Salem Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga akiwa Mtoto wa 6 wa Mwalimu Emmanuel Chamshama na Bibi Sarah Shemshi.Mwili mwili wake umepumzishwa leo tarehe 06/03/2025 katika makaburi yaliyopo katika eneo la Kanisa Kuu Lushoto.Sehemu ya historia ya Bibi Elfriede Sebastian Kolowa inaeleza kuwa.

Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi moja  ya MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA (PROJECT COORDINATOR) kwa vijana wote  (Wakristo) 

NAFASI NA WAJIBU WA MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA (PROJECT COORDINATOR).

1.1 CHILD AND YOUTH DEVELOPMENT CENTER COORDINATOR (CYDC)- MRATIBU WA KITUO CHA MAENDELEO YA MTOTO NA KIJANA.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ambaye pia ni msimamizi Mkuu wa mali za Dayosisi amesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kinacho milikiwa na KKKT-DKMs na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), makubaliano yanayolenga kuboresha na kukuza taaluma na tafiti katika vyuo hivyo.