
Tarehe 28/11/2024 Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki walipata nafasi ya kutembelea kituo cha Malezi bora ya Watoto Irente (Irente Children's Home) pamoja na Shule ya Watoto wasioona (Irente School for the Blind) ambapo walipata nafasi yakuona miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ukarabati wa Majengo pamoja na ujenzi wa Green House.

Shule ya Watoto wasioona Irente (Irente School for the Blind). Shule ina miradi midogomidogo ukiwemo mradi wa kilimo cha mbogamboga ndani ya greenhouse ambapo kumekuwepo na greenhouse moja kwa miaka mingi. ambayo tayari ina mazao na nyingine mpya iko kwenye maandalizi ya kuoteshwa mazao kwa lengo la kufanya shughuli za kujitegemea na kuiingizia shule/kituo kipato.

Mradi mpya wa Greenhouse ambao ni kati ya miradi iliyokuwa kwenye mpango mkakati wa Shule kwa miaka kadhaa pamoja na mpango mkakati wa mwaka 2024. Baada ya kushirikisha wadau tofautitofauti hatimaye Mama Helga Walter kutoka Ujerumani aliahidi kusaidia kutafuta fedha ili kupatikana greenhouse. Bingo Enviromental Foundation of Lower Saxony ndio wafadhili wa mradi huu wa Greenhouse.