HABARI KWA UFUPI

Wakristo wamekumbushwa kuendelea kumtumaini na kumtegema Mungu pale wanapo pata mafanikio katika maisha yao kwani katika dunia ya sasa wapo waliofanikiwa na mara baada ya kupata mafanikio hayo wakamsahau Mungu na kufuata njia zao, na kuamini kuwa mafanikio hayo wameyapata kwa nguvu zao.

Hayo yamesemwa na Jackson Msafiri Mbilu wakati akihubiri kwenye Ibada ya Jumapili ya leo tarehe 09/02/2025 iliyoongozwa na Vijana katika Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.” Ndugu zangu inasikitisha lakini ni uhalisia kuwa sisi binadamu sikuhizi tukifanikiwa katika maisha yetu, hatutaki kuwakumbuka kabisa wale waliotufikisha katika mafanikia. Tunawageuzia kisogo na kujifanya hatuwajui.”Alisema.

Ameongeza kuwa neno la Mungu ndiyo silaha na ngao katika maisha  lakini  inasikitisha katika ulimwengu wa sasa kuona watu wamekuwa wavivu wa kusoma neno la Mungu na kuna watu wanaoishi bili kumwamini mungu ameongeza kuwa wapo Wakristo, wanaofika kanisani  ilimradi tu waoneka  kuwa wamefika kanisani ili wakiulizwa na wengine waseme wameenda kanisani, hali inayopelekea kushindwa kujibu hata maswali marahisi yanayohusu Biblia. 

 Hata hivyo Jackson amewahimiza  Wakristo kushiriki Ibada katika ukamilifu wake ili kuzivuna baraka za Mungu amesema litrugia sio Ibada kamili, muda wa mahubiri sio Ibada kamili au nzima, muda wa sadaka sio Ibada nzima, matangazo sio Ibada nzima bali Ibada kamili ni ile ambayo umeshiriki kuanzia mwanzo hadi baada ya mnada na hapo ndio unaweza ukasema umeshiriki Ibada katika ukamilifu wake.Yesu ndio tumaini letu sisi wanadamu tunapaswa kumfuata yeye, na kwakupitia maandiko matakatifu ya Mungu tunasikia neno lake na mafundisho yake sauti ya huyu Yesu tutaisikia kila siku kama tutapenda kukaa nyumbani mwa Bwana kulisoma Neno la Mungu kila siku na kila saa.  

 Katika Dayosisi yetu, KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Ibada zimeongozwa na vijana na katika Usharika wa Kanisa Kuu Ibada iliongozwa na Edison Kisaka pamoja na Jackson Mbilu.

Jackson Mbilu ambaye ndiye aliyehubiri ni Mtoto wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Dkt.Msafiri Joseph Mbilu ,ameeleze jinsi alivyokuwa anajiandaa na Ibada ya leo.“Moja wapo ya maandalizi Nilipokuwa ninaandaa haya mahubiri, Sasa pale nyumbani kwetu chatllon kuna ka ofisi cha baba ambayo anatumiaga kuandaa mahubiri sasa na mimi nikiwa ninayaandaa ya kwangu nikasema naenda kukaa pale pale. kwenye kiti kile kile angalau na mimi nipate upako na kujuwa nini cha kusema”. Alisema Jackson.