Leo tarehe 3 Novemba 2020 kumefanyika mahafali ya 31 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Lwandai inayomilikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, ambapo wanafunzi 50 (wa kike 26 na wa kiume 24) wamehitimu. Mgeni rasmi katika mahafali haya alikuwa ni Mchungaji Peter Bendera (Mkuu wa Dinari ya Kaskazini).
Mahafali haya yalifana sana yakipambwa na vishirikisho mbalimbali toka kwa wahitimu na wanafunzi wengine. Mchungaji Peter Bendera aliwaasa wahitimu kuendelea kujitahidi kusoma kwa bidii, na kwamba wazingatie maadili mema katika maisha yao. Pia aliwatakia baraka katika mitihani yao inayotazamiwa kuanza Novemba 23-2020. Kulifanyika pia maombezi maalumu kwa wahitimu, kidato cha pili, walimu na wanafunzi wote yaliyoongozwa na wachungaji.
Lwandai Secondary school held their 31st Form Four Graduation today, 3rd of November 2020. The Guest of honor was Rev. Peter Bendera (Dean, Northern Deanery). In his speech Rev. Peter Bendera urged Form Fours who expect to sit for their National Exams later this month to study hard and maintain their good ethical life. In this graduation pastors did special prayers for form fours and form twos for their forthcoming National exams later this month.